Ghasia Zazidi Kupamba Moto Haiti, Bendelea Zasubiri Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu

Ilichapishwa miezi 10 iliyopita
  Pexels

Tarehe 16 Machi 2024, ghasia zimeendelea kupamba moto nchini Haiti, kati ya makundi ya wahalifu na polisi. Ghasia hizi zimekuwa zikiendelea kwa muda mrefu, huku hali ya vurugu na fujo ikiendelea kushuhudiwa nchini humo. Waziri mkuu Ariel Henry anatarajiwa kujiuzulu siku ya Jumatatu, lakini makundi haya ya wahalifu hawasubiri kujiuzulu kwake.

Mapema mwezi huu, serikali ilitangaza hali ya dharura, lakini hali nchini Haiti imeendelea kuzorota zaidi. Katika mitaa ya mji mkuu, Port-au-Prince, kulizuka moto na barabara zikazuiliwa usiku wa Ijumaa. Pia kulikuwa na mapigano kati ya makundi ya wahalifu na polisi.

Waziri mkuu mwenye umri wa miaka 74, Henry, alitangaza kutoka Puerto Rico kwamba atajiuzulu siku ya Jumatatu. Bado haijajulikana nani atamrithi. Kiongozi maarufu wa genge, Jimmy Chérizier, alisema kujiuzulu kwake ni “hatua ya kwanza tu” katika vita ambavyo makundi ya wahalifu yanaendesha.

“Mwaziri mkuu Henry anajiuzulu, lakini hali ya dharura ya kisiasa inaendelea. Wanasiasa wanapaswa kuchukua jukumu la kuandaa upya nchi,” alisema raia mmoja wa Haiti katika eneo la Caribbean siku ya Ijumaa, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters. Awali, mamia ya wafungwa walitoroka baada ya mashambulizi ya makundi ya wahalifu chini ya uongozi wa Chérizier.

Related news