Mgogoro Haiti: Marekani Yajiondoa Wafanyakazi wa Ubalozi Kutokana na Ghasia za Magenge

Ilichapishwa miezi 10 iliyopita

Ghasia za magenge zinazoendelea nchini Haiti zimeongeza shinikizo kwa Waziri Mkuu Ariel Henry, na kuzidisha hali ya kibinadamu inayoendelea kuzorota. Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, magenge yenye nguvu yanayokusudia kuipindua serikali ya mpito ya Waziri Mkuu Henry yamezua hali ya mtafaruku nchini Haiti kwa takriban siku kumi zilizopita. Ndege zote za abiria zimesitisha safari zake.

Ghasia hizo zimepamba moto mwishoni mwa mwezi Februari, ambapo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, magenge yanadhibiti takribani asilimia 80 ya mji mkuu, Port-au-Prince. Bado haijulikani ni watu wangapi wameathirika na ghasia hizo. Inakadiriwa kuwa karibu nusu ya watu wapatao milioni 11 wa Haiti wanakabiliwa na njaa kali.

Henry, ambaye ni daktari wa upasuaji wa ubongo mwenye umri wa miaka 74, alichukua usukani wa serikali baada ya kuuawa kwa Rais Jovenel Moïse nyumbani kwake mnamo Julai 2021. Tangu wakati huo, hakuna uchaguzi uliofanyika, na Haiti haina Rais wala Bunge. Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 300,000 wamelazimika kuhama makazi yao nchini Haiti kutokana na ghasia za magenge katika miaka ya hivi karibuni.

Marekani Yajiondoa

Kufuatia ghasia hizo, jeshi la Marekani limerudisha nyumbani wafanyakazi wasio wa lazima wa ubalozi wake nchini Haiti na kuongeza hatua za kiusalama katika ubalozi huo. Taarifa hiyo imetolewa na Southcom, ambayo ni sehemu ya jeshi la Marekani inayosimamia operesheni za kijeshi katika eneo hilo.

Related news